Map na Usafi wa Mazingira (MUM) ni mradi wa miaka mitano (Agosti 2021 – Agosti 2026) unaofadhiliwa na Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) kwa Tanzania.
MUM inakaribisha maombi (Vidokezo vya Dhana) yanayoelezea bidhaa na huduma kutoka kwa makampuni madogo madogo yaliyosajiliwa, wamiliki pekee, na wajasiriamali kushughulikia mahitaji kwa kuwalenga wenye kipato duni katika mnyororo wa thamani ya usafi wa mazingira na usafi kupitia kusaidia ubunifu kwa makampuni madogo kuyawezesha kutoa huduma na bidhaa zinazofaa na / au huduma ambazo zinaweza kuwezesha dhana ya efanya mwenyewe’ na watu wenye kipato duni zaidi -catika jamii zinazolengwa na MUM. Tafadhali tembelea tovuti https:// tetratech.force.com/ard kwa maelezo zaidi na pia kuweza kupakua tangazo la wito wa maombi (Request for Applications MUM-RFA-004).
Waombaji wote wanaovutiwa wanaweza kuwasiliana na kitengo cha Ruzuku cha MUM kwa kutumia baruapepe kwa: tanzaniamum.grants@ tetratech.comkuomba nyaraka kamili ya maombi ya ruzuku, au wanaweza kupakua moja kwa moja kutoka katika tovuti ya Tetra Tech grants portal (https://tetratech.force.com/ard).
Tarehe ya mwisho ya maombi ni Machi 28, 2023.
Wito huu hauifungi kisheria programu ya Maji na Usafi wa Mazingira (MUM) kushirikiana na makampuni yoyote madogo, mmiliki pekee, au mjasiriamali yeyote. Hakuna ahadi inayofanywa, ama iliyoonyeshwa au kudokezwa, kumfidia mwombaji kwa gharama atakayoingia katika maandalizi au uwasilishaji wa maombi yake.