TANGAZO LA ZABUNI YA KAZI YA UKUSANYAJI WA ADA YA UZOAJI WA TAKA NGUMU, UZOAJI WA TAKA NGUMU NA KU FANYA USAFI KATIKA MJI MIDOGO YA MAGHANG, DONGOBESH NA HAYDOM KWA KIPINDI CHA KUANZIA MEI 2021 HADI JUNI 2021
Halmashauri ya wilaya Mbulu katika mwaka wa fedha 2020/2021 inakusudia kutoa KAZI YA UKUSANYAJI WA ADA YA UZOAJI WA TAKA NGUMU NA UZOAJI WA TAKA NGUMUNAKUFANYA USAFI katika miji midogoya Dongobesh, Maghang na Haydom kuanzia mwezi Mei 2021 hadi mwezi Juni 2021. Mkurugerizi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu anawatangazia Wananchi, Makampuni na Taasisi mbalimbali kuleta maombi ya Utoaji wa huduma hiyo.
MASHARTI YA KUOMBA ZABUNI ZA UTOAJI HUDUMA YA UZOAJI TAKA NA UKUSANYAJI WA USHURU WA TAKA NGUMU
1.Koteheni inapatikana kwa kulipa ada( fedha hizi hazitarudishwa) ya shilingi 100,000 (Mia moja elfu tu) kwa kila zabuni. Nyaraka za. zabuni zinapatikana kwenye ofisi ya Ununuzi na Ugavi, Halmashauri ya wilaya ya Mbulu iliyopo Dongobesh.
2. Zingatia kuwa fomu ya maombi ya zabuni inajazwa na kusainiwa na mwenye uhalali wa kisheria (Power of Attorney) katika zabuni hii.
3.Mwombaji wa zabuni endapo atachaguliwa, atalazimika kuilipa Halmashauri fedha taslimu Tsh. 5,000,000/= (Milioni sitini Tu) ambayo ni dhamana ya kazi anayopewa kabla ya kuanza kazi. Mshindi wa zabuni hataruhusiwa kuanza kazi ya kukusanya ushuru kabla ya kulipa fedha yote ya dhamana.
4. Mfumo wa kielektroniki (POS) ndio utakaotumika kukusanyia ushuru na mtoa huduma atalamizimika kuwasilisha kwa halmashauri mapato yote aliyokusanya kwa kutumia (POS) kwa kipindi husika na baada ya hapo halmashauri itawajibika kumlipa mtoa huduma kiasi kinachostahili, hivyo Mwombaji (mtoa huduma) lazima aoneshe ni asilimia ngapi atastahili kulipwa kama ma Ii po kwa ajili ya kazi hii ambazo atarejeshewa kila atakapowasilisha makusanyo halmashauri
5. Mwombaji awasilishe zabuni halisi na nakala mbili.
6. Zabuni ijazwe vizuri, iwekwe kwenye bahasha iliyofungwa kwa La kiri baada ya kujazwa na wazabuni na juu ya bahasha iandikwe kwa HERUFI KUBWA ZABUNI ILIYOOMBWA bila kuwekwa a lama yoyote ya kumtambulisha muombaji.
7. Mwombaji asiwe mtumishi wa serikali/shirika la umma.
8. Zabuni zitawasilishwa kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu makao makuu ya Halmashauri, Ofisi ya manunuzi na Ugavi iliyopo Dongobesh.
9. Mwisho wa kuwasilisha maombi ni tarehe 05/07/2021 saa nne kamili asubuhi na zabuni zitafunguliwa ndani ya dakika 30 baada ya muda wa kuwasilisha zabuni kuisha.
10. Zabuni zote ziambatane na kiapo cha dhamana ya zabuni (Tender securing declaration) kwa kuzingatia fomati iliyoainishwa katika kitabu cha zabuni.
11. Waombaji wanakaribishwa kuhudhuria wakati wa ufunguzi katika ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri iliopo Makao makuu ya Halmashauri ya wilaya (Dongobesh).
12. Zabuni ambazo zitachelewa kwa muda uliopangwa na zabuni zitakazotumwa kwa mtandao (email,fax) hazitapokelewa.
13. Halmashauri hailazimishwi kwa njia yoyote kukubali om bi lolote.
14. Mwombaji aandike barua ya maombi ya zabuni na kuiwasilisha kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri, Ofisi ya Ununuzi na Ugavi, Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, S.L.P 74, Mbulu.
15. Mwombaji atakayeshindwa masharti haya atakuwa amejiondoa mwenyewe kwenye mchakato mzima wa zabuni. 16. Mwombaji aambatishe Cheti cha usajili wa kampuni au kikundi.
17. Mwombaji awe na Leseni ya biashara.
18. Mwombaji aoneshe Wafanyakazi wenye uwezo wa kukusanya ada ya uzoaji taka kwa kutumia (POS).
19. Mwombaji awe na Wafanyakazi wakufanya usafi katika miji midogo ya Haydom, Maghang na Dongobesh.
20. Mwombaji aoneshe Vifaa vya kazi ya uzoaji wa taka ngumu alivyonavyo.
21. Uzoefu wa kazi ya uzoaji wa taka ngumu.
Florence Kundy
KAIMU MKURUGENZI MTENDAJI,
HALMASHAURI YA WILAYA MBULU .