utumishi

MTENDAJI WA KIJIJI III – 1 POST

WhatsApp
Twitter
Email
LinkedIn
Instagram

 Halmashauri ya Wilaya ya Longido

Afisa Masuuli na mtendaji mkuu wa serikali ya kijiji;

Kusimamia ulinzi na usalama wa raia na mali zao, kuwa mlinzi wa amani na msimamizi wa utawala bora katika kijiji;

Kuratibu na kusimamia upangaji wa mipango ya maendeleo ya kijiji;

Katibu wa mikutano na kamati zote za Halmashauri ya kijiji;

Kutafsiri na Kusimamia Sera, Sheria na Taratibu;

Kuandaa taarifa ya utekelezaji wa kazi katika eneo lake na kuhamasisha wananchi katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoa njaa, umaskini na kuongeza uzalishaji mali;

Kiongozi wa wakuu wa vitengo vya klitaalam katika kijiji;

Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na nyaraka za kijiji;

Mwenyekiti wa kikao cha wataalam waliopo katika kijiji;

Kupokea, kusikiliza na kutatua malalamiko na migogoro ya wananchi;

Kusimamia utungaji wa Sheria Ndogo za kijiji; na 

Atawajibika kwa Mtendaji Mkuu wa Kata.

QUALIFICATION AND EXPERIENCE

Kuajiriwa mwenye Elimu ya kidato cha Nne(IV) au Sita (VI) aliyehitimu mafunzo ya Astashahada/Cheti katika moja ya fani zifuatazo: Utawala,Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya Sanaa kutoka Chuo Cha Serikali za Mitaa Hombolo, Dodoma au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.

APPLICATION TIMELINE: 2024-06-12 2024-06-28

APPLY NOW

WhatsApp
Twitter
Email
LinkedIn
Instagram

Related