NYANZA CO-OPERATIVE UNION (1984) LTD
TANGAZO LA ZABUNI
Nyanza co-operative union (1984) Ltd inawatangazia zabuni za kupanga kwenye majengo yake kwa ajili ya matumizi mbalimbali kama vile hotel, Hospitali, Lounges, Bar and cafeteria, huduma za kibenki na matumizi mengine ya ofisi kwa ajili ya Taasisi, kampuni na mashirika mbalimbali. Maeneo yanayo tangazwa ni kama ifuatavyo;
A: JIJINI MWANZA (Pamba Hostel)
- Jengo lipo mjini mkabala na jengo la PSSSF na Maktaba ya mkoa wa Mwanza katika barabara ya station (station road) karibu kabisa na Mzunguko wa sanamu ya samaki.
- Huduma zote za msingi, ikiwa ni pamoja na maji na umeme ni za uhakika
- Jengo lina eneo la kutosha kwa ajili ya maegesho ya magari
- Jengo ni imara na madhubuti (structurally and esthetically)
B: WILAYANI UKEREWE (Pamba Hostel)
- Jengo lipo karibu na Benki ya NMB Ukerewe, karibu kabisa na eneo la bandari ya Nansio Ukerewe.
- Huduma za umeme na maji zinapatikana katika jengo
- Eneo la kutosha kwa ajili ya maegesho ya magari
- Jengo ni imara na madhubuti (structurally and esthetically)
Bahasha za zabuni zifungwe kwa rakili na kuandikwa juu, Zabuni za kupanga Jengo (Pamba hostel Jijini Mwanza/ Pamba hostel wilayani Ukerewe).
Ada ya zabuni isiyorudishwa ya Tsh 100,000/= italipwa kwa kila zabuni kupitia CRDB Benki akaunti namba 01J1007418502 NCU(1984) LTD – Na Pay in slip iletwe jengo la NYANZA CO-OPERATIVE UNION (1984) LTD Makao Makuu Mwanza lililoko bararabara ya Kenyatta au iambatanishwe kwenye nyaraka za zabuni.
MAMBO YA KUZINGATIA:
Jina kamili la mzabuni, anuani ya Posta, Namba ya Simu, maha-li anapopatikana au anakoishi (makazi), pamoja na viambatanisho vyenye kuthibitisha uwezo wa kulipa kodi ya jengo ipasavyo.
Wazabuni wanashauriwa kufika na kukagua maeneo yaliotangazwa kwa msaada wa maofisa wetu walio karibu na maeneo hayo katika muda wa saa za kazi.
Tangazo la Zabuni litakuwa ndani ya siku kumi na nne (14) Kuanzia tarehe 15-07-2021 na mwisho wa kutuma Maombi ni tarehe 28-07-2021 saa 3.00 Asubuhi. Zabuni zitafunguliwa tarehe 28-07-2021 saa 5:00 Asubuhi katika ukumbi mdogo (Mabenga Hall) wa jengo la NYANZA CO-OPERATIVE UNION (1984) LTD makao Makuu mwan-za lililoko barabara ya Kenyatta. Mzabuni au mwakilishi anatakiwa kuhudhuria ufunguzi wa zabuni.
Uongozi wa NCU (1984) Ltd Haufungwi na kanuni yoyote juu ya kukubaliwa au kukataa zabuni yoyote ile ya chini au ya juu isipoku-wa uamuzi wake ni wa mwisho.
Hatupokei zabuni zilizo tumwa kwa FAX au EMAIL.
Mzabuni anatakiwa kutaja kiwango cha kodi ya jengo husika atakacholipa.
Zabunl zote zitumwe kwa:
MENEJAMKUU
NCU (1984) LTD
P.O. BOX 9, MWANZA
TELL: 028 2500299