Nafasi ya kazi :- MTEKNOLOJIA WA SAMAKI DARAJA LA II (FISH TECHNOLOGIST II)
Wizara ya Mifugo na Uvuvi-UVUVI
3 Positions
Duties and Responsibilities
- Kutoa ushauri juu ya utayarishaji, uchakataji, ukaushaji na uhifadhi wa samaki na mazao ya uvuvi;
- Kukagua na kusimamia ubora wa mazao ya uvuvi na mwani kulingana na viwango vya kitaifa ana kimataifa;
- Kusimamia na kushauri kuhusu Kanuni za udhibiti ubora wa mazao ya uvuvi na mwani;
- Kudhibiti ubora wa samaki katika mialo, masoko, viwanda na maghala;
- Kudhibiti usafi katika maeneo ya kupokelea samaki na mwani;
- Kukagua viwanda vinavyochakata, maghala ya kuhifadhia mazao ya uvuvi na vyombo vya usafirishaji wa mazao ya uvuvi kulingana na “HACCP” (Hazard Analysis Critical Control Point);
- Kuhakiki nyaraka mbalimbali za uzalishaji na usafirishaji wa mazao ya uvuvi na mwani; na
- Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wa Kitengo zinazohusiana na fani yake.
Qualifications
- Kuajiriwa wenye mojawapo wa Shahada za fani za Fish Technology, Marine Biology and Applied Microbiology, Fisheries Sciences and Microbiology kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam; Sayansi ya Chakula (Food Technology and Microbiology) kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine au sifa inayolingana na hiyo kutoka vyuo vikuu vingine vinavyotambuliwa na Serikali.
RemunerationTGS DApplication Period08/12/2025 - 23/12/2025APPLY NOW https://portal.ajira.go.tz/view-advert/iNEJLYZqxljReHhF9Ugj1g%3D%3D