Nafasi ya kazi :- Auction: Zabuni ya ununuzi wa trekta aina ya John Deere 5503 at So They Can Tanzania November 2026

So They Can_847.png

Wito wa zabuni: Uuzaji wa trekta

ZABUNI NAMBA: STC/TZ/ADV/2026/02

Shirika la So They Can Tanzania linategemea kuuza trekta, mali ya shirika. Mauzo ya trekta hilo yanazingatia mahali trekta lilipo na hali yake ya sasa “Kama Lilivyo, Mahali Lilipo”

Maelezo ya trekta

  • Aina ya trekta: John Deere

  • Namba ya Usajili: T 958 CDY

  • Mwaka wa Kutengenezwa: 2012

  • Modeli: 5503

  • Chesesi Namba: PY5503E003356

  • Hali ya Injini: Nzuri

     
  • Aina ya Mafuta: Dizeli

  • Mfumo wa Giabox: Manual

  • Rangi ya Nje: Kijani

  • Hali ya Tairi: Nzuri

  • Bima: Inaisha 18 Desemba 2026

Masharti na vigezo vya uuzaji

1. Kama Lilivyo, Mahali Lilipo

Trekta litauzwa kulingana na hali yake ya sasa. Waombaji wanashauriwa kulikagua kabla ya kuwasilisha maombi yao ya manunuzi.

2. Uwasilishaji wa maombi ya manunuzi

Maombi lazima yawasilishwe katika ofisi za So They Can Tanzania, Nyumba namba 1, Mtaa wa Sinza, Nyunguu, Babati, kwenye bahasha iliyofungwa ikiwa imeandikwa “Maombi ya ununuzi wa trekta – T 958 CDY” au maombi yatumwe kwa barua pepe kwenda [email protected].

Mwisho wa kutuma maombi hayo ni Jumatatu tarehe 16 November 2026 saa 11:00 jioni.

3. Masharti ya malipo

Mwombaji atakayepitishwa kununua trekta husika atatakiwa kufanya malipo kwa asilimia 100% ya bei ya manunuzi, kupitia akaunti ya benki ya So They Can Tanzania ndani ya siku saba baada ya kupokea taarifa ya kukubaliwa ombi la manunuzi, Taarifa hii itatolewa tarehe 21 Novemba 2026

4. Kodi, ada za kisheria, na gharama za uhamisho

Mnunuzi atatakiwa kulipia gharama zote zinazohusiana na uhamisho wa umiliki wa trekta, kodi husika, ada za uhamisho, na gharama ya kadi mpya ya usajili.

5. Uchukuaji wa trekta

Mnunuzi atatakiwa kuichukua trekta ndani ya siku tano (5) baada ya kukamilisha malipo, na uhamisho wa umiliki, na kufikisha nakala ya kadi ya umiliki mpya kwenye ofisi za So They Can Tanzania.

Sera ya kutokuvumilia rushwa, ufisadi, na ughushi

So They Can Tanzania inaendeshwa chini ya sera ya kutokuvumilia kabisa (zero-tolerance) kuhusiana na rushwa, ufisadi, ughushi, njama za siri. Jaribio lolote kutoka kwa mwombaji, wakala wao, au mwakilishi, kutoa ahadi, au kutoa zawadi yoyote, rushwa, kamisheni, au kivutio cha kifedha kwa mfanyakazi au mwakilishi yeyote wa So They Can Tanzania kitasababisha kuondolewa mara moja kwa zabuni hiyo.

Njama kati ya waombaji ili kupanga bei au kuchezea matokeo ya mchakato huu wa zabuni zimepigwa marufuku vikali na zitasababisha kukataliwa kwa moja kwa moja na uwezekano wa kuripotiwa kisheria. Shaka au ushahidi wowote wa shughuli za ughushi, maelezo ya uongo, au vitendo vya kifisadi vitasababisha kusitishwa mara moja kwa mkataba wa uuzaji.

Ufichuaji / Uripoti wa Siri

Waombaji wanaoshuhudia au kushuku tabia yoyote ya kifisadi au ya ughushi inayohusiana na zabuni hii wanaweza kuripoti kwa siri kupitia [email protected].

Ukaguzi na maswali

Ukaguzi wa trekta

Mwombaji anaweza kuomba kukagua trekta kupitia namba za mawasiliano hapo chini.

  • Tarehe za kukagua: 9 hadi 13 November 2026

     
  • Muda: Saa 03:00 asubuhi – saa 11:00 jioni

  • Eneo: Ofisi ya So They Can Tanzania, Na.1, Mtaa wa Sinza, Nyunguu, Babati, Manyara

Namba za mawasiliano So They Can Tanzania

John Jonas Mwakipesile, Afisa Mawasiliano

Simu: +255 687 128 570

Noel Patrick Mndalila, Dereva

Simu: +255 753 937 175

Barua Pepe Rasmi: [email protected]

Tamko la uaminifu la mwombaji

Wakati wa uwasilishaji wa maombi ya ununuzi wa trekta, waombaji wanatakiwa kusaini kauli hii fupi pamoja na maombi yao:

“Mimi/Sisi tunathibitisha kuwa nimesoma/tumesoma, nimeelewa/tumeelewa, na ninakubali/tunakubali kuzingatia Sera ya So They Can Tanzania Dhidi ya Rushwa, Ufisadi, na Ughushi. Mimi/Sisi tunathibitisha kuwa maombi haya yamefanywa bila makubaliano yoyote ya awali, njama, au mipango na mwombaji mwingine yeyote au mfanyakazi yeyote wa So They Can Tanzania.”

Sahihi: ___________________________

Jina: ______________________________

Tarehe: ____________________________